Friday, May 17, 2013

Ilikuwa hivyo na itaendelea kuwa hivyo ya kwamba binadamu ndiye haswa mbadilishaji wa haya mazingira.Na kama hutolikubali hili basi umepotea, mana siku zote utakuwa ni mwenye kubadilishwa na mazingira ya aina yoyote ile utakayokutana nayo,kila majaribu ya mazingira masafi na machafu yatakumeza wewe. ukikutana na viongozi wa dini na hata viongozi wa dhambi pia utawafata mana umeyapa nafasi mazingira yakuchagulie njia ya kupita badala ya wewe kuyatambua na kuyaamulia yaweje? aidha yawe na ukuta maji mengi yasiharibu bustani yako au ukate miti ili kupata njia ya kupita wewe na familia yako. mambo sasa yamebadilika. watu tumeibebea booonge la mbereko hizi dhambi zetu ili tu, zisije zikatushinda kuzibeba tena hasa pale tunapotaka na za ziada pia. Jamani tupiganie uhuru ili kupata nafasi ya kuuonesha umma ya kwamba tunaweza kufanya maendeleo katika jamii hii iliyomsahau mwanamke na kumgeuza ni chombo cha starehe tu na si vinginevyo.
Isiwe ni uhuru wa kuonesha na hata sisi pia dhambi twaziweza tena sambamba ama bega kwa bega na nyinyi wanaume.Zamani wasichana walishinda na mama zao majikoni kujua nini hasa anachopaswa kukijua kule jikoni. Lakini leo wanashinda na kaka zao au hata wenye umri sawa na baba zao kwenye vilabu vya ulevi kujifunza yale ambayo hata ukiwauliza wao wenyewe wasingependa vizazi vyao vivifanye.mwanamke ni stara ya nje ya nyumba yako, jikoni na chumbani.tubadilike basi jamani eh? thamani ya mwili wako na matendo yako inapandishwa na wewe mwenyewe.hata akununulie magari na mavazi ya thamani bado huna tofauti na mfuko wa taka... mana nje hapana shida sababu kuna vutia sana tu, lakini ndani una mafunza na mabuu kama kaburi,na hayo mavazi au magari ni maficho tu ili yasionekane mauozo yako,lakini ndani unateketea.Sio imani za kidini bali hata utamaduni wetu ambao ulikuwepo hata kabla ya hao waliotusambazia hizi imani ngeni, pia unakemea vikali suala la heshima na thamani ya kujitambua we ni nani na ni nini hasa majukumu yako.akuambiaye anakupenda na huu ndio uwanja wa wapendanao kidhati.

No comments:

Post a Comment