Ataruka na kuvimba ikibidi hata kutamani kukutemea mate yenye sumu kama nyoka eti tu sababu uko mbali kidogo na yeye, mana laitani ungelikuwa karibu kiasi basi ungelikwishapigwa kibao cha shavuni, na yooote hayo sababu umemuita "MZINIFU"....... Ni sawa si jina lake alilopewa na wazazi wake, lakini jamani hiyo si ndo sifa yako kwasababu huwa unazini? na si peke yako ! mana hata afundishaye huitwa mwalimu, mpenda Nchi yake yeye ni Mzalendo, anayefata maamrisho ya M/mungu huitwa Mchamungu au muumini na pia kuna na hawa wakina Walevi na kadhalika sasa iwaje wewe ufure hadi ufikie kupasuka yakheee......Hadi tunakasirishwa na sifa za mabaya yetu sababu haifai kuwa wachafu wakufikia kiwango hiko. Na hii ni kuonesha kwa kiasi gani sisi ni wadhaifu wa kupindukia tunapokuwa katika mapambano dhidi ya tamaa za miili yetu, Hivi kwa nguvu zako na
akili yako na kila neema na uwezo ambao umebarikiwa na aliyekuumba,
pamoja na ahadi uliyoiweka mbele ya huyohuyo ambaye unadai unamuabudu,
Unathubutu kumsaliti na kuisaliti ndoa yenu iliyofungwa mbinguni? Mumeo
ni hodari maskini, anajitahidi hata kukubali kudhalilika ilimradi
familia ipate yaliyobora, basi huoni aibu kumsaliti? Mkeo usiku kucha
anakesha kumuomba Mungu mfanikiwe huku akivumilia na kuamini huenda
kesho mwenzangu atafanikisha tutoke kwenye maisha ya ufukara na
mitihani, basi kiumbe gani usiyekuwa na hata alama au kivuli tu cha
huruma juu ya mke wako? Sikufichi utakachoweza wewe ni kukimbia tu, tena
kwasababu miguu ni yako una uhuru wa kuitumia utakavyo, Lakini kamwe
hutoweza kujificha sababu macho yatakayokufichua ulipo si yako na huwezi
kuyaamrisha yasikutazame ulipojificha. kama kweli unajihisi vibaya kwa
kuitwa jina la sifa yako mbaya inayonuka basi haraka jiepushe na
upumbavu uitunze na kuinyenyekea familia yako, kama kweli umemaliza
kuyasoma haya maneno ninaamini bado upendo ndani yako upo. Tafadhali
onesha upendo wa dhati kwa mwenzako.............
No comments:
Post a Comment