Monday, June 3, 2013

 Rahma na wifi yake kwenye karo la mipango.
 mara baada ya ndizi mbuziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Ahh my beloved little sister i real realy love you so much.

 KULALA NI SEHEMU MUHIMU YA BINADAMU
TENA NI AFYA BASI TULALE TUKUE, TUPUMZIKE NA TUPATE AFYAAAAAaaaaaa.....

Saturday, May 18, 2013

Ataruka na kuvimba ikibidi hata kutamani kukutemea mate yenye sumu kama nyoka eti tu sababu uko mbali kidogo na yeye, mana laitani ungelikuwa karibu kiasi basi ungelikwishapigwa kibao cha shavuni, na yooote hayo sababu umemuita "MZINIFU"....... Ni sawa si jina lake alilopewa na wazazi wake, lakini jamani hiyo si ndo sifa yako kwasababu huwa unazini? na si peke yako ! mana hata afundishaye huitwa mwalimu, mpenda Nchi yake yeye ni Mzalendo, anayefata maamrisho ya M/mungu huitwa Mchamungu au muumini na pia kuna na hawa wakina Walevi na kadhalika sasa iwaje wewe ufure hadi ufikie kupasuka yakheee......Hadi tunakasirishwa na sifa za mabaya yetu sababu haifai kuwa wachafu wakufikia kiwango hiko. Na hii ni kuonesha kwa kiasi gani sisi ni wadhaifu wa kupindukia tunapokuwa katika mapambano dhidi ya tamaa za miili yetu, Hivi kwa nguvu zako na
akili yako na kila neema na uwezo ambao umebarikiwa na aliyekuumba, pamoja na ahadi uliyoiweka mbele ya huyohuyo ambaye unadai unamuabudu, Unathubutu kumsaliti na kuisaliti ndoa yenu iliyofungwa mbinguni? Mumeo ni hodari maskini, anajitahidi hata kukubali kudhalilika ilimradi familia ipate yaliyobora, basi huoni aibu kumsaliti? Mkeo usiku kucha anakesha kumuomba Mungu mfanikiwe huku akivumilia na kuamini huenda kesho mwenzangu atafanikisha tutoke kwenye maisha ya ufukara na mitihani, basi kiumbe gani usiyekuwa na hata alama au kivuli tu cha huruma juu ya mke wako? Sikufichi utakachoweza wewe ni kukimbia tu, tena kwasababu miguu ni yako una uhuru wa kuitumia utakavyo, Lakini kamwe hutoweza kujificha sababu macho yatakayokufichua ulipo si yako na huwezi kuyaamrisha yasikutazame ulipojificha. kama kweli unajihisi vibaya kwa kuitwa jina la sifa yako mbaya inayonuka basi haraka jiepushe na upumbavu uitunze na kuinyenyekea familia yako, kama kweli umemaliza kuyasoma haya maneno ninaamini bado upendo ndani yako upo. Tafadhali onesha upendo wa dhati kwa mwenzako.............

Friday, May 17, 2013

Ilikuwa hivyo na itaendelea kuwa hivyo ya kwamba binadamu ndiye haswa mbadilishaji wa haya mazingira.Na kama hutolikubali hili basi umepotea, mana siku zote utakuwa ni mwenye kubadilishwa na mazingira ya aina yoyote ile utakayokutana nayo,kila majaribu ya mazingira masafi na machafu yatakumeza wewe. ukikutana na viongozi wa dini na hata viongozi wa dhambi pia utawafata mana umeyapa nafasi mazingira yakuchagulie njia ya kupita badala ya wewe kuyatambua na kuyaamulia yaweje? aidha yawe na ukuta maji mengi yasiharibu bustani yako au ukate miti ili kupata njia ya kupita wewe na familia yako. mambo sasa yamebadilika. watu tumeibebea booonge la mbereko hizi dhambi zetu ili tu, zisije zikatushinda kuzibeba tena hasa pale tunapotaka na za ziada pia. Jamani tupiganie uhuru ili kupata nafasi ya kuuonesha umma ya kwamba tunaweza kufanya maendeleo katika jamii hii iliyomsahau mwanamke na kumgeuza ni chombo cha starehe tu na si vinginevyo.
Isiwe ni uhuru wa kuonesha na hata sisi pia dhambi twaziweza tena sambamba ama bega kwa bega na nyinyi wanaume.Zamani wasichana walishinda na mama zao majikoni kujua nini hasa anachopaswa kukijua kule jikoni. Lakini leo wanashinda na kaka zao au hata wenye umri sawa na baba zao kwenye vilabu vya ulevi kujifunza yale ambayo hata ukiwauliza wao wenyewe wasingependa vizazi vyao vivifanye.mwanamke ni stara ya nje ya nyumba yako, jikoni na chumbani.tubadilike basi jamani eh? thamani ya mwili wako na matendo yako inapandishwa na wewe mwenyewe.hata akununulie magari na mavazi ya thamani bado huna tofauti na mfuko wa taka... mana nje hapana shida sababu kuna vutia sana tu, lakini ndani una mafunza na mabuu kama kaburi,na hayo mavazi au magari ni maficho tu ili yasionekane mauozo yako,lakini ndani unateketea.Sio imani za kidini bali hata utamaduni wetu ambao ulikuwepo hata kabla ya hao waliotusambazia hizi imani ngeni, pia unakemea vikali suala la heshima na thamani ya kujitambua we ni nani na ni nini hasa majukumu yako.akuambiaye anakupenda na huu ndio uwanja wa wapendanao kidhati.
Legendary Bi Maumbile: ameitwa bi maumbile sababu haishi kuugua viungo vyake ndo wakamtunga hilo jina la Maumbile.ni mtu wa maneno mengi na mapenzi ya ndugu zake,udhaifu wake ni umbea tu! ila si mlaumu saana mana si mnafki bali ni mbea tu, yaani huwa anafikisha taarifa upande wa pili kabla ya muda rasmi wa kufikisha taarifa hiyo au ruhusa toka kwa wahusika haswa wa taarifa hiyo, lakini hazidishi chumvi {Bigup Bi Maumbile} msemo wake mkubwa ni "KULA MAVI, KUNYA MAVI" hana maana ya kukufuru au kumtia mtu kinyaa bali hapa chini ya jua wote ni sawa haijalishi UMRI, MALI, CHEO, JUU, CHINI, JINSIA, KABILA, KOO au FAMILIA utokayo woooooote sisi ni sawa.......na ni kweli mana hakuna mbora kati yetu ispokuwa yule anayemcha M/mungu


Whatever difficulty you face, there are time-tried ways you can listen your way through.
Because listening is the doorway to everything that matters. It enlivens the heart the way
breathing enlivens the lungs. We listen to awaken our heart. We do this to stay vital and
alive.
Mark Nepo
Si pakiwa na raha tu bali hata kipindi cha shida pia yatupasa kuwa karibu tena ikibidi hata kuzidi ya hapa, mana hivyo ndivyo familia inabidi iwe,huu uwe mnyororo ambao maadui dhaifu na imara wote washindwe kuukata.